Arusha wapanda miti 510
MKUU wa Mkoa wa Arusha ,John Mongella amewaongoza wakazi wa Jiji la Arusha katika zoezi la upandaji miti zaidi ya 510 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka Miwili ya Rais Dk, Samia Suluhu Hassan kuwepo madarakani.
Katika hotuba yake Mongella aliyoitoa Shule ya Arusha School amesema, katika kipindi cha miaka miwili imefanya mambo mengi makubwa ikiwepo ujenzi wa mdarasa kwa kila wilaya,ujenzi wa vituo vya afya,zahanati, hospitali za wilaya pamoja na kutoa vifaa tiba kwa sekta ya afya.
Mongella amesema pia kwa kipindi cha miaka miwili nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Mwalimu,Nyerere,ujenzi wa reli ya kisasa Dar es Salaam kwenda Dodoma,ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato Dodoma,ujenzi wa Meli Mpya ya kisasa ya Mv.Victoria,daraja la Kigongo-Busisi Mwanza pamoja na kukamilika kwa ununuzi wa ndege kubwa ya mizigo.
Kwa upande wa Mkoa wa Arusha katika kipindi cha miaka miwili,Mkoa kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliweza kukusanya maduhuli jumla ya sh,533,684,695,18 sawa na asilimia 107.13 ya lengo la makusanyo waliopangiwa.
Hii ilitokana na mazingira mazuri ya kibiashara yaliyowekwa na serikali humu Halmashauri za Mkoa wa Arusha zilfanikiwa kuchangia miradi ya Maendeleo kiasi cha 50,428,931,974 sawa na 86.9% ya makusanyo.
Vile vile Halmashauri hizo zimefanikiwa kutoa Mikopo ya 10% kutokana na mapato ya ndani kwa Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu jumla ya sh,6,831,640,918/=.
Maadhimisho ya Miaka Miwili ya Rais Dk,Samia Suluhu Hassan tangu kuwepo madarakani 19,Machi,2021 hadi 19,Machi,2023 Kimkoa yalianza tarehe 13,Machi,2023 kwa kuzindua Kitabu cha mafanikio yake pia shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwemo michezo(Mabonanza) na hatimaye leo tarehe 19,Machi,2023 kwa hitimisho la upandaji miti kuenzi juhudi za Rais kwenye suala la utunzaji Mazingira nchini.