Arusha wasitisha vibali uhamisho walimu
KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha, Misaille Mussa, amesitisha vibali vya uhamisho wa walimu kwa kisingizio cha mazingira mabovu, ili kuweza kudhibiti uhaba wa watumishi wa serikali katika Halmashauri ya Ngorongoro.
Vibali hivyo vilivyositishwa ni kwenye idara ya afya na elimu, badala yake watatoa vibali vya uhamisho wa ndani ya halmashauri peke yake kusudi kukidhi mahitaji ya upungufu wa walimu katika baadhi ya shule.
Uamuzi huo umekuja baada ya viongozi hao akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kupitia na kujadili hoja 38 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka wa fedha 2021/2022.
Vibali hivyo vimesitishwa kwa kisingizio cha mazingira mabovu ili kuweza kudhibiti uhaba wa watumishi wa serikali katika halmashauri ya Ngorongoro kwenye idara ya afya na elimu, badala yake watatoa vibali vya uhamisho wa ndani ya halmashauri peke yake, kusudi kukidhi mahitaji ya upungufu wa walimu katika baadhi ya shule.