Asanteni Serengeti Girls

Asanteni Serengeti Girls

ASANTENI Serengeti Girls! Ndiyo wanastahili kupewa shukurani mabinti hao wa timu ya Taifa ya Tanzania ya wasichana chini ya umri wa miaka 17.

Hatua hiyo inatokana na kufuzu Robo Fainali ya Kombe la Dunia linaloendelea nchini India, baada ya usiku huu kutoka sare ya bao 1-1 na Canada katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi.

Kwa mazingira hayo Japan ambayo leo imefunga Ufaransa mabao 2-0, imeongoza Kundi D ikiwa na pointi tisa, ikifuatiwa na Tanzania yenye pointi nne, ikiwa imeshinda mchezo mmoja, sare mmoja na kupoteza mmoja.

Advertisement