Asasi yabeba tuzo viwango bora

KAMPUNI ya Asas inayohusika usambazaji na uuzaji wa maziwa imetunukiwa tuzo ya heshima kwa viwango vya ubora wa bidhaa.

Tuzo hizo zimefanyika Dar es Salaam ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa kampuni hiyo kushinda tuzo hiyo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Abdallah Asas alisema kila mwaka maelfu ya bidhaa kutoka sekta tofauti zinaamuliwa dhidi ya ya vigezo vitatu vya muhimu vya Superbrands ubora kuaminika na utofauti.

Advertisement

“Nichukue nafasi hii kuwashukuru waandaji wa tuzo hizi za Superbrand, kushinda tuzo hii ni ishara tosha ya juhudi za uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa maziwa yetu nchini kuendelea kuwa bidhaa muhimu katika jamii.

“Tuzo hii ina maana kubwa kwa wateja wetu kwa kuendelea kuiamini ASAS kwa zaidi ya miaka 80, tunawashukuru sana na tutaendelea kuwapatia huduma za viwango vya ubora wa hali ya juu,” alisema Abdallah.