Ashauri wahitimu ufundi kujiajiri mitandaoni

MSHAURI wa masuala ya kifamilia Anti Sadaka amewataka wahitimubwa elimu ufundi wa ushonaji kutumia mitandao ya kijamii kwaajili ya kukuza ubunifu wao na sio kufanya vinginevyo.

Akizungumza na wahitimu hao katika kongamano lililoandaliwa na chuo cha Voice of Eagle yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam,  Sadaka  alisema kwa sasa biashara imehamia kwenye mitandao hivyo kila kitu wanachokifanya lazima wakitangaze.

Sadaka alisema wasiogope kuajiliwa wanapopata nafasi hiyo, kwakuwa kupata nafasi ya kufanya kazi kwa mtu ni sawa na kuongezea ujuzi katika ubunifu wake.

“Sio mnashona ili mradi kuuza sura mtandaoni, ila fanyeni kwaajili ya kukuza jina na ubunifu wenu” alisema.

Mkurugenzi wa chuo hicho Meshaki Robart alisema amekuwa akiwasafirisha wabunifu wake kwenda katika nchi tofauti ili kupata ujuzi na kubuni nguo tofauti.

Alisema alishawahi kuwapeleka nchini Kenya kwaajili ya kuongeza ujuzi na wabunifu wengine, lakini bado wanajipanga kwenda katika nchi zingine kwaajili ya kuongezea ujuzi.

“Zaidi ya ubunifu wa mavazi ya kushona lakini pia tumekuwa tukitoa mafunzo mengine, kama kilimo na computer.Hii tunafanya ili watu watoke na taaluma na kusaidia raisi Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa Taifa”.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x