Ashinda kwa kishindo uwenyekiti jumuiya ya wazazi

Julius Kaondo ameshinda kwa kishindo kwa kura 565 kati ya kura 652 zilizopigwa katika nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Mkoa wa Mtwara.

Uchaguzi huo umefanyika jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu kawaida (TTC) Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo kwa upande wa Mpinzani wa Mwenyekiti huyo ambaye ni Juma Nachembe alipata kura 58 kati ya kura hizo 652 zilizopigwa na kura 5 ziliharibika huku kura halali zikiwa 647.

Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara Alhaji Rajabu Kundya amepongeza namna ambayo zoezi hilo la uchaguzi lilivyofanyika kwani lilikuwa la utulivu, amani kubwa kutokana hakukuwa na dalili zozote zenye kupelekea vurugu au vitendo vya rushwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo aliyechaguliwa katika uchaguzi huo “Mimi niwashukuru Sanaa ndugu Wajumbe kwa hili kubwa mlilolifanya la kunipa dhamana hii kubwa naomba tu ushirikiano wenu ili tuzidi kulisukuma mbele gurudumu hili la maendeleo kupitia Jumuiya ya Wazazi”,

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x