Asilimia 16 wagundulika na Presha kwa siku mbili
DAR ES SALAAM: Jana ilikuwa ni siku ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani ambapo asilimia 16 ya watu waliofanya uchunguzi katika kambi ya uchunguzi ya siku mbili wamegundulika kuwa na tatizo hilo.
Kambi ya uchunguzi iliyoanza Mei 16 na 17,2024 ilihudhuriwa na watu 2014 ambapo kati yao watu 32 walikuwa na shikizo la juu la damu.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani,Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ,Dk Tatizo Waanne amesema watoto waliofanyiwa uchunguzi ni 32 ambapo kati yao 16 walikutwa na matatizo ya kiafya.
“Leo ni siku ya shikizo la juu la damu ambapo Magonjwa ya moyo yanachangia vifo vyote Duniani kwa asilimia 30 hususani shinikizo la damu huu ni ugojwa ambao kama unamtindo bora wa maisha unaweza kuzui visababishi,”alisema.
Dk Waanne amesema mtu anapopatikana na tatizo anaweza kupata madhara katika mwili kama moyo kuwa mkubwa,kiharusi,matatizo ya figo huku sababu kubwa ni shikizo la damu.
Isome pia https://habarileo.co.tz/presha-ya-macho-kiini-cha-upofu/
“Kambi hii ni muhimu kama tungekuwa hatujafanya hawa watu wasingejua na sasa wanaweza kuchukua hatua.
Ameeleza kuwa visababishi hazijulikani lakini tafiti zinaonesha wanaokunywa pombe kupita kiasi wanaweza kupata,matumizi ya bidhaa za tumbaku kama ugoro,shisha,sigara, kutokufanya mazoezi, ulaji usiofaa na uzito mkubwa.
“Tuna kambi ya matibabu mara kwa mara ili kufikia wananchi wengi zaidi na tuna wataalmu wengi wanashiriki na zoezi ni endelevu kila baada ya muda fulani tunafanya nawashauri watu wawe na tabia ya kupima afya na kubadili mtindo wa maisha kwasababu matibabu haya ni ghali ,”amesisitiza.
Kwa upande wake Mkazi wa Temeke Mikoroshini, Hamisi Gadawi amesema anashukuru kwa kupata huduma za vipimo na dawa bure kwani angaanda kwingine Angela hela.
“Nimeona niitumie nafasi hii nimeangaliwa na madaktari bingwa nimepata matibabu na dawa nashukuru kama ningeenda kwingine ningechajiwa hela nawashauri Wananchi wengine wafike kupima afya zao ni bure wasiogope kupima ni kitu cha kawaida na muhimu mimi Leo nimepata dawa,”ameeleza.
Naye Chusiku Sulemani amesema kuwa amegundulika na kisukari na shinikizo la juu la damu na Madaktari wamemshauri vyakula anavyotakiwa kula.
“Nina sukari na presha na madakatri wamenishauri kuacha kunywa chai,kutotumia sukari na matunda yenye sukari na nilikuwa sijui kama ninasukari nimefika hapa nimeambiwa ipo na nimepata na dawa bure.