Asilimia 65.6 kidato cha kwanza hawajaripoti

KAGERA : JUMLA ya wanafunzi 21,267 sawa na asilimia 34.4 ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2024 wameanza masomo yao ndani ya wiki moja huku asilimia 65.6 wakiwa bado awajaripoti shule kuanza masomo.

Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Khalifa Shemahonge amesema kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni 61,831 kati ya hao wasichana ni 31,559 na wavulana ni 30,272

Amesema kuwa kati ya wanafunzi waliojitokeza kuripoti shuleni ndani ya wiki moja ya kwanza wasichana ni 111,22 sawa na asilimi 35.24 na wavulana ni 10,146 sawa na asilimia 33.52

Alitaja wilaya ambazo wanafunzi bado hawajafika shuleni kuwa ni wilaya ya Biharamulo wanafunzi wamefika kwa asilimia 20,wilaya ya Karagawe wanafunzi wamefika kwa asilimia 23 na wilaya ya Ngara wanafunzi wamefika kwa asilimia 24

Aidha wilaya ambayo inaongoza wanafunzi kufika kwa wingi shuleni ni Manispaa ya Bukoba asilimia 49 ikifatiwa na wilaya ya Karagwe asilimia 48

Viongozi mbalimbali wa serikali na chama mkoani Kagera kwa kipindi cha wiki moja wamefanya ziara za kuhamasisha wazazi kuwapeleka kwa wakati watoto wao ili wasichelewe kuanza masomo yao.

Katibu tawala mkoani Kagera Toba Nguvilla alikagua shule mbalimbali na kuangalia namna watoto walivyoanza masomo ambapo alitumia muda wake kuongea na wakuu wa shule na kukemea tabia za kutuma michango mbalimbali isiyo na tija na kufukuza wanafunzi ambao wanamapunfu huku akiomba watoto waachwe huru wasome.

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima alitangaza Opresheni maalum ya kukamata wazazi kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama endapo watoto wao watafikia tarehe 22 January bila kufika shuleni na kuanza masomo yao.

Habari Zifananazo

Back to top button