WANAFUNZI 11,271 ambao ni sawa na asilimia 71.51 mpaka sasa kwa mwaka huu 2024, wameripoti kidato cha kwanza katika Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Joina Nzali amesema hayo alipozungumza na Mwandishi wa habari hii.
Joina amesema kwa sasa idadi ya wanafunzi walioko sekondari za serikali ni 41,203 katika shule 36.
Pia amesema katika shule za msingi kwenye darasa la kwanza walitaraijiwa kuandikishwa wanafunzi 22,574, lakini mpaka sasa walioandikishwa ni 19,473 ambao ni sawa na asilimia 86.26.
“Jumla ya shule za msingi za serikali ni 69 ambazo zina jumla ya wanafunzi 105,983,” amesema.
Mkuu huyo wa Kitengo Joina amesema katika madarasa ya awali walitarajia kuandikishwa wanafunzi 24,612 lakini mpaka sasa wameandikishwa 7,893 sawa na asilimia 32.
Kwa ujumla amesema wanafunzi 38,637 wameanza masomo yao Januari mwaka huu, katika Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam.