Asilimia 77.3 ya Vijiji Kagera Vyaunganishwa na Umeme wa REA

KAGERA: Vijiji 512 kati ya Vijiji 662 vya Mkoa wa Kagera ambayo ni sawa na asilimia 77.3 ya vijiji vya mkoa huo vimefikiwa na huduma ya umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Vijiji hivyo vimefikishiwa umeme wa REA ikiwemo Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, REA Awamu ya Pili na REA Awamu ya Kwanza huku vijiji 150 ambavyo bado havijaunganishwa na huduma hiyo vitaunganishwa kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, ambapo tayari mkandarasi anaendelea na kazi za mradi huo.

Aikungumza kuhusu utekelezaji wa miradi ya REA, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huyo, Hassan Saidy alisema Shilingi bilioni 80 imetolewa na Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa umeme vijijini mkoani humo.

“Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini ndani ya Mkoa wa Kagera imewekeza Sh bilioni 80 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kusambaza umeme vijijini, na hivi ninavyoongea ndani ya mkoa huu kuna miradi mitano inatekelezwa,” amesema Saidy wakati wa hafla wa uwashaji wa umeme Kijiji cha Mubaba, wilayani Biharamulo.

Aidha, viongozi na wananchi wa mkoa huo wamemshukuru Rais Samia Hassan kwa kuwawezesha kupata umeme wa uhakikia, ambao utafungua fursa mbalimbali katika maeneo yao.

“Tangu umeme wa REA umeingia kijijini, tayari watu wameshanunua ‘fridge’, watu wameshaanza kutafuta mashine za umeme kwa ajili ya kusaga, hata mashine za kutoa ‘photocopy’ tumeanza kupata,” amesema Diwani wa Kata Murusagamba iliyopo Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera, Sudi Mkubira.

Naye Mfanyabiashara wa Mchele katika Kijiji cha Mubaba wilayani Biharamulo, Kalebo John amesema: “Umeme wa REA umetusaidia kupata mashine za kukoboa mpunga za umeme, kabla ya kuja umeme huu tulikuwa tukikoboa mpunga kwa kutumia mashine za mafuta ambazo zilikuwa zinasababisha mchele kuwa mweusi hivyo tulikuwa tukikosa wateja.”

Katika kuhakikisha kila kijiji mkoani humo kinapata umeme, kwa sasa REA inatekeleza miradi mitano ambayo ni Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Mradi wa Kupeleka umeme Pembezoni mwa Miji, Mradi wa ujazilizi, Mradi wa Kupeleka umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo, na Mradi wa Kupeleka umeme kwenye Vituo vya Afya na Pampu za Maji.

Aidha, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko yupo kwenye ziara ya kuwasha umeme katika vijiji vya mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora na Singida.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
EmeraldEartha
EmeraldEartha
2 months ago

I’m currently generating over $35,100 a month thanks to one small internet job, therefore I really like your work! I am aware that with a beginning capital of $28,800, you are presently making a sizeable quantity of money online.( q33w)
Just open the link——->> http://Www.SmartCareer1.com

AnneThomas
AnneThomas
2 months ago

My last salary was $8,750 only worked 12 hours a week. My longtime neighbor estimated $15,000 and works about 20 hours for seven days. I can’t believe how blunt he was when I looked up his information.
.
.
Detail Here—————————————————————->>>  http://Www.BizWork1.Com

Lisa D. Nelson
Lisa D. Nelson
2 months ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 2 months ago by Lisa D. Nelson
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x