Asilimia 85 waripoti kidato cha kwanza Tanga Jiji

WANAFUNZI 6745 sawa na asilimia 85, wameripoti shule kwa àjili ya kuanza kidato cha kwanza katika shule za serikali, huku wanafunzi zaidi ya 1250 hawajaripoti mpaka sasa katika Jiji la Tanga.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa, wakati wa ziara yake ya ufuatiliaji wa maendeleo ya uandikishaji wa wanafunzi kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za sekondari jijini Tanga.

Amesema kuwa mpaka sasa shule ambazo zipo katika kata za mjini zimekuwa hazifanyi vizuri, kwa kuwa na uandikishaji wa chini ya asilimia 60.

“Natoa wiki moja idara ya elimu msingi na sekondari sambamba na watendaji wa mitaa kuja  na taarifa za wapi watoto wengine ambao mpaka sasa wameshindwa kuripoti shule na sababu zao,” amesema DC Mgandilwa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya amepiga marufuku michango ya aina yoyote, ambayo inachangwa katika shule bila ya kufuata utaratibu wa kibali kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa wilaya.

 

Habari Zifananazo

Back to top button