Asilimia 96 Waviu wamefubaza makali

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema asilimia 94.4 ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (Waviu) wanatambua hali zao na kati yao asilimia 98.8 wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU na Ukimwi.

Ummy ameyasema hayo leo Mei 12,2023 bungeni mjini Dodoma akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo, ambapo amesema pia asilimia 96.6 ya Waviu wamefubaza makali ya ugonjwa huo.

“Tumeangalia ufanisi wa dawa tumefanya vipimo kwa wagonjwa 309,263, asilimia 96.6 ya waliofanyiwa vipimo wameonekana kwamba Virusi vya Ukimwi vimefubazwa.” Amesisitiza

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x