Askari Polisi 5 mbaroni kwa usafirishaji wahamiaji haramu

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia askari watano wa Jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia.

Akizungumza kwa njia ya simu na HabariLeo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga leo Novemba 3, 2022 amesema askari hao walikuwa wakiwavusha raia hao wa Ethiopia kwenda nchini Malawi kupitia mpaka wa Kasumulu uliopo wilayani Kyela.

Kamanda Kuzaga, ametoa wito kwa askari kuacha kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Habari Zifananazo

Back to top button