Askofu Laban atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari

Askofu Laban atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari

CHUO cha ANCCIU, kilichopo Texas, Marekani  kimemtunuku  Shahada ya Heshima ya Udaktari, Askofu Mkuu wa Makanisa ya News Harvest Afrika, Laban Ndimubenya kutokana na mchango wake katika jamii hususani majukumu ya dini.

Dk Laban ametunukiwa shahada hiyo katika hafla iliyofanyika kanisani kwake, New Harvest, mjini Mpanda Mkoa wa Katavi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali wakiongozwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Hassan Rugwa.

Advertisement

Akisoma wasifu wa Askofu Laban, mwakilishi wa chuo hicho, Prof. Benezer Mwang’ombe, ametaja sababu nyingine ni hatua aliyoipiga katika elimu na mchango wake kwa kanisa na jamii kwa ujumla kiroho na kijamii.

Kwa upande wake Dk Laban, amesema ni heshima kubwa kwake kwa chuo cha All Nations Christian Church International University  (ANCCIU) cha Marekani  kutambua mchango wake katika utumishi kwa jamii na hatimaye kuona inafaa kutunukiwa shahada hiyo ya heshima ya udaktari.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *