Aslay yupo tayari kufanya kazi na Fella

MSANII, Aslay Isihaka amesema hatokataa endapo Saidi Fella atataka wafanyekazi tena kama menaja wake sababu yeye ndiye aliyemfikisha hapo alipo.

Aslay anasema yeye ni kama  mchezaji mpira endapo timu yeyote inamtaka na ina maslahi mazuri mchezaji anasaini hivyo naye endapo Fella atataka asaini asimamiwe tena kama meneja wake hatokataa.

“Kama Fella anataka nisaini kufanya naye kazi kwa nini nikatae mimi kama mchezaji mpira akitaka nisaini nitasaini,” amejibu Aslay.

Advertisement

Aslay ameongeza kwamba Fella ni baba yake mwenye mchango mkubwa katika mafanikio yake ya kimuziki hivyo hawezi kukataa kufanyanaye kazi.

“Mkubwa Fella ni baba yangu amenikuza hadi leo nilipo ndiyo maana leo nipo hapa kufurahia usiku wake wa tuzo alizopata huko Afrika Kusini na namwamini katika muziki anaousimamia na namisi vitu vingi sana kutoka kwake,” amesema Aslay.

Hata hivyo Aslay aliombwa kusikiliza nyimbo mbili za wasanii wapya wanaounda kundi la ‘Yamoto Band’ kundi ambalo yeye ndiye msanii muasisi.

1 comments

Comments are closed.