Atabiri mtikisiko baraza la mawaziri

NABII Philbert Paschal ametoa unabii na kusema kuwa muda wowote kuanzia sasa kutatokea mtikisiko kwenye mabadiliko yanayokuja ya Baraza la Mawaziri.

Pia, amewasihi wale watakaoondolewa kwenye nafasi za uongozi kumshukuru Mungu kwa kipindi walichoongoza na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ili nchi iendelee mbele.

Nabii Philbert wa Kanisa la Bwana Yesu kwa Mataifa Yote lililopo Tabata Kinyerezi ametoa unabii katika ibada ya Jumapili ya ‘My Friend set me free’.

Amesema,  muda wowote kuanzia sasa Wizara zitabadilika na kutakuwa na mtikisiko kwenye mabadiliko hayo huku akisisitiza kuwa waziri mkubwa (bila kumtaja jina) ataondolewa kwenye nafasi ya uongozi.

” Waliozoea kumlia mama timing nina sema mama (Rais Samia) asomeki, na hawatamsoma tena na Mungu ameruhusu. Sio muda mrefu Wizara zitabadilika na Baraza la mawaziri linaenda ku-shake(kutikiswa), hii ni kutoka kwa Mungu.”

Na nitoe tahadhari kama ulipewa dhamana ya kuwa kiongozi Serikalini au kiongozi wa jamii au kampuni ukiondolewa usilaumu, shukuru Mungu kwa sababu uongozi ni kupokezana hivyo usitafute kuumia au kufarijiwa ona ni sehemu ya kazi njema umefanya. “Amesisitiza

Nabii Philbert ameongeza: “muda si mrefu kuna watu wataondolewa kwenye Wizara zao, naona kiti cha waziri aliyemkubwa, sijui ni waziri gani ila elewa ni waziri aliyemkubwa. Sisemi tuliombee hili ila mapenzi ya Mungu yakatimie.”

Kuhusu siasa, Nabii Philbert amesema pia kutakuwa na mtikisiko kutokana na kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya vyama vikubwa viwili vya siasa vya Chama cha Mapinduzi(CCM) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).

” Naona kutatokea mgawanyiko mkubwa sana ndani ya vyama vikubwa vya siasa ambao utatengeneza shake(mtikisiko) kati ya CCM na Chadema na kimoja wapo kitagawanyika sana. Tuwaombee hao ili Mungu atengeneze amani.”

Aidha, Nabii Philbert amewaomba wakristu husani waumini wa Kanisa la Bwana Yesu kwa Mataifa Yote kuuendelea kumuombea Rais Samia hekima na busara ya Mungu ikatawale na upendo wake ukadhihirike kwa jinsi anavyoonekana.

Pia tumuombee Rais Samia, asubuhi, mchana na usiku ili akapate watendaji wazuri wa kumsaidia kazi anayoifanya kwa nchi yetu.”

Nabii Philbert amesema kuanzia mwezi Februari watanzania watatulia na kuwa na furaha na kusisitiza kuwa wengi wa wakurugenzi wataondolewa kabisa katika nafasi zao na wale wasiotarajiwa wanapewa nyadhifa mbalimbali.

Habari Zifananazo

Back to top button