Ataka maelezo Sh mil 600 ziivyotumika ujenzi wa shule

ARUSHA; Longido. Naibu Waziri wa Madini Dk  Steven Kiruswa, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido mkoani Arusha, amekataa kuchangia ujenzi wa shule ya Msingi Mundarara, mpaka apate maelezo ya kina matumzi ya fedha Sh mil 600 zilizotumwa na Serikali katika ujenzi wa shule hiyo.

Kiruswa amesema hayo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea ujenzi wa madarasa nane, ofisi ya utawala,vyumba vitatu vya maabara na vyoo havijamaliziwa na nyumba ya mwalimu mkuu haijajengwa, milango hakuna na sakafu haijamaliziwa na tayari zimetumika zaidi ya shilingi milioni 576.

Amesema ameambiwa fedha zilizobaki katika akaunti ni shilingi milioni 8 tu na bado shule haijakamilika kabisa.

Amesema katika kata zingine jimboni Longido,  fedha za serikali zilizopelekwa katika kata kiasi kama hicho kilichopelekwa Shule ya Msingi Mundarara, kila kitu kimekamilika.

Naibu Waziri amesema kutonana hali hiyo hawezi kuchangia chochote, hadi ufanyike ukaguzi maalumu wa matumizi ya fedha zote zilizotumika na apate majibu, kwani Kamati ya Ujenzi wa shule hiyo haikushirikishwa.

Habari Zifananazo

Back to top button