Ataka mitaala kuwezesha mahitaji ya soko

SERIKALI imeelekeza kuwa mapitio ya mitaala ya programu za maendeleo ya jamii na uhandisi ujenzi na maendeleo ya jamii yalenge kuandaa wataalamu watakaokidhi mahitaji ya soko la ajira na kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili wawe na mchango kwenye jamii.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk John Jingu wakati wa kufungua warsha ya mapitio ya mitaala ya programu za maendeleo ya jamii na Uhandisi Ujenzi na Maendeleo ya Jamii ngazi ya Astashahada na Stashahada.

Mitaala hii inafanyiwa mapitio baada ya kuwa imetumika kwa kipindi cha miaka mitano ifikapo Juni 2023.

Alisema mitaala ni nyenzo muhimu katika utoaji wa mafunzo na kuwa mapitio hayo ni hatua ya msingi kutokana na mabadiliko yanayochangiwa na ukuaji wa kasi wa teknolojia na mabadiliko ya tamaduni.

Dk Jingu alisema pia mapitio ya mitaala yanapaswa kuzingatia mahitaji ya soko la ajira, mahitaji ya kada husika na jamii na vipaumbele ya nchi.

Habari Zifananazo

Back to top button