Ataka ubunifu mifumo ya Tehama

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi ameagiza Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), kufanya utafiti ili kuleta ubunifu wa mifumo ya Tehama itakayowezesha Taifa kufanikiwa kwenye sekta ya viwanda  ,biashara na uwekezaji.

Agizo hilo amelitoa leo jijini Arusha katika ufunguzi wa kikao kazi cha tatu cha  Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kilichowakutanisha wakuu wa taasisi mbalimbali, wakurugenzi, makatibu Tawala na wadhamini wa mkutano huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah (wa pili kushoto) akifuatilia mada katika kikao kazi cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) mjini Arusha leo (Picha zote na Veronica Mheta).

Amesema shughuli nyingi zinazofanyika duniani hivi sasa zinaendeshwa kwa Tehama, hivyo endapo ubunifu utafanyika utaleta tija kwa nchi haswa katika sekta za viwanda, biashara na uwekezaji.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Utumishi , Dk,Laurian Ndumbaro ameagiza wakurugenzi, wakuu wa taasisi kuachana na matumizi ya makatarasi katika vikao vyao, badala yake watumie vishikwambi ili kuendana na kasi ya teknolojia

Habari Zifananazo

Back to top button