Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tanga, Shaymaa Kwegyir, amewaasa vijana kuacha tamaa badala yake wasome kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari za Kata ya Mkinga mkoani Tanga.