Ataka viongozi wa dini kushawishi waumini kulipa kodi ya pango

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula amewaomba viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu zaidi kwa Watanzania ili waweze kuona umuhimu wa kulipa kodi ya pango ambayo imeondolewa tozo kwa msamaha wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mabula amesema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini kwenye mahafali ya sita kwa wahitimu wa ngazi ya juu ya madaktari na maprofesa iliyodhaminiwa na Chuo cha Outreach Care International Marekani yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mipango kilichopo Dodoma.

Alisema viongozi wa dini wana uwanja mpana wa kuwaelimisha Watanzania kuhusu kuona umuhimu wa kulipa kodi hiyo ya pango ambayo kwa hivi sasa Rais Samia ameweza kuiondoa kwa msamaha ili wale wote wanaodaiwa walipe bila kushurutishwa na serikali.

Advertisement

“Niwaombe viongozi wangu wa madhehebu ya dini endeleeni kuisaidia serikali katika kutoa elimu kwa watu wenu huko kwenye nyumba za ibada kwa ajili ya kulipa hiyo kodi ya pango ambayo imetolewa msamaha na rais ili Watanzania waitoe bila kushurutishwa,” alisema.

Naye Mkuu wa mafunzo ya viongozi hao, Profesa Rejoice Ndalima amewataka viongozi wa dini kujiongeza zaidi katika kuitafuta elimu ya kutosha ili waweze kufanya kazi zao vizuri kwenye maeneo yao. Aidha, amewataka viongozi wao wa dini kuwa ni watu wa kuipenda nchi kwa ajili ya kuleta maendeleo yatakayoisaidia kuwepo kwa amani na kuendelea kuwepo kwa umoja na mshikamano utakaojenga taifa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *