‘Atakayemkwamisha Rais, ama zake ama zetu’

MBUNGE wa Tarime Vijijini Mwita Waitara, amesema wamejipanga vizuri kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hadi sasa kwa majimbo yote mkoani Mara wamefikia asilimia 98.

Amesema uchaguzi wa mwakani wa serikali za mitaa watashinda kwa kishindo na uchaguzi mkuu unaotarajiwa  kufanyika mwaka 2025 wamejipanga kufanya vizuri.

“Nawaomba watu wa Mara na Tanzania, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeweka mipango ya kuona wananchi wanapata maji, barabara, elimu, afya na vijana kupata ajira, hakuna mtu yeyote ambaye anapita katikati kumkwamisha Rais Samia na tukimuona ama zake ama zetu,” amesema Waitara.

Amesema Rais  Samia Suluhu Hassan yupo imara wanamuunga mkono na serikali ipo imara.

 

Habari Zifananazo

Back to top button