ATCL yapata hasara Sh Bil. 35

KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL), imepata hasara ya Sh bilioni 35.

23 katika mwaka wa fedha 2021/22. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza.

Akiwasilisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,  2022, CAG Charles Kichere amesema katika ripoti yake imeonesha mwaka wa fedha 2020/21, ATCL ilipata hasara ya Sh bilioni 36.18.

Amesema ripoti yake imebaini katika ATCL walijiwekea lengo la ndege zinazochelewa iwe ni asilimia 8 lakini kupitia ukaguzi wake umebaini ndege hizo kuchelewa kwa kwa asilimia 25.

Habari Zifananazo

Back to top button