ATCL yapata hasara Sh Bil.56

DODOMA: MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limepata hasara  ya Sh Bilioni 56.64 sawa na ongezeko la asilimia 61 kutoka hasara ya Sh Bilioni 35.24 kwa mwaka uliopita.

Akiwasilisha ripoti ya utendaji kazi wa serikali na Mashirika mbalimbali ya umma, CAG Kichere amesema kwa upande wa  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hasara imepungua kutoka Sh Bilioini 205.95 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi Sh Bilioni 156.77 kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Aidha amesema michango ya wanachama imeongezeka kwa asilimia 14.6 na matumizi yameongezeka kwa asilimia 10.

Habari Zifananazo

Back to top button