SHIRIKA la Ndege Tanzania limetangaza uwepo wa changamoto za mabadiliko ya ratiba za ndege kutokana na uchache wa ndege zilizobaki uliosababishwa na kuchelewa kwa upatikanaji wa injini mbili za Airbus A220-300 baada na injini zake kupata matatizo.
Katika taarifa yao iliyochapishwa Aprili 12, 2023 na kutolewa leo, ATCL imeeleza kuwa injini mbadala zinazotakiwa kutolewa na mtengenezaji Pratt & Whitney (P&W), zilitarajiwa kuwasili mwanzoni mwa mwezi Aprili 2023.
“Kutokana na changamoto hizi, tunalazimika kutoa huduma kwa ratiba inayobanana sana ili kukidhi mahitaji makubwa ya wateja wetu”. Imeeleza taarifa hiyo.
“Wakati tunashughulikia changamoto hizi kwa haraka, tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza, kampuni ya ndege itaendelea kuhakikisha inatoa huduma bora ili kufikia matarajio ya wateja wetu”.imeeleza taarifa hiyo”.