ATE wasifu tozo nafuu Osha

CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kimeipongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa jithada kubwa iliyofanya ya kupunguza tozo za Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).

Ofisa mtendaji mkuu wa chama hicho , Wakili Suzanne Ndomba Doran amesema hayo wakati akitoa salamu za Chama hicho kwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahali pa kazi duniani mjini Morogoro

Doran amesema licha ya jitihada hizo ,chama hicho kinaendelea kupendeza kushushwa kwa gharama zinazotozwa mathalani tozo za upimaji wa afya za wafanyakazi na gharama za kufanya ukaguzi.

Licha ya hayo, Doran ameiomba serikali kupitia upya na kuweka utaratibu mzuri wa muda wa kufanya ukaguzi katika maeneo ya kazi .

Ofisa Mtendaji mkuu wa chama hicho amesema mazingira salama ya kazi yanachochea uzalishaji na mahisiano mazuri mahala pa kazi.

Amesema sheria ya afya na usalama mahala pa kazi ya m waka 2003 inamtaka mwajiri kutengeneza mazingira yenye afya na usalama mahali pa kazi .

“ ATE ikiwa ndiyo sauti ya waajiri wote nchini kwa kushirikiana na wadau imekuwa mstari wa mbele kuhumiza waajiri kuzingatia na kutekeleza makatwa ya sheria hii “ amesema Doran

Amesema , ATE inaahidi kuendeleza ushirikiano wao katika kutoa elimu kwa waajiri ili kulinda afya na usalama mahala pa kazi ili kuleta tija na ufanisi mahala pa kazi.

Habari Zifananazo

Back to top button