Meshack Binari (34), mkazi wa Kijiji cha Katambike, Kata ya Ugala Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi ameuawa, wakati akijaribu kumzuia Ramadhan Pongera (85), mkazi wa Kitongoji cha Uvuvi aliyetaka kumbaka jirani yake.
–
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani, amesema mtuhumiwa Ramadhan Pongera, amekamatwa na polisi na upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea.
–
Amesema tukio hilo lilitokea Julai 13, 2023 saa moja asubuhi Kijiji cha Katambike, ambapo mtuhumiwa Pongera alitaka kuingia katika chumba cha jirani yake (jina tunalihifadhi) kwa lengo la kumbaka, ndipo Binari alipomzuia kutekeleza kitendo hicho, hivyo kujeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni.
–
Baada ya tukio hilo Meshack alipelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi na asubuhi siku iliyofuata alifariki akiwa bado anaendelea na matibabu hospitalini.
Comments are closed.