Auawa katika shambulizi la msafara wa raia

WATU wenye silaha wanaoshukiwa kutoka kwa wahamaji wa Misseriya wa Sudan, wameshambulia msafara wa raia na kumuua mtu mmoja katika eneo la Utawala la Abyei.

Waziri wa Habari wa Abyei, Ajak Deng Miyan alisema katika tukio hilo la juzi Jumapili, watu wengine watatu akiwemo mwanamke walipata majeraha katika shambulio hilo la kuvizia katika lori mbili za Toyota pick-up zilizokuwa zimebeba raia kando ya barabara ya Abyei.

“Leo Jumapili (juzi), tarehe 18 Septemba, majira ya asubuhi, watu kutoka kundi lenye silaha la Agaira Misseriya walivamia na kushambulia magari mawili ya Toyota katika eneo la Kol-nyang,” ilisema taarifa.

Msemaji wa eneo hilo la mpakani lenye matatizo alisema mmoja wa raia waliojeruhiwa, ambaye alikuwa katika hali mbaya alikimbizwa katika hospitali ya Todac UNISFA katika mji wa Abyei.

“Eneo la Utawala la Abyei linalaani shambulizi hili la kinyama kwa muda mrefu iwezekanavyo na kutoa wito kwa UNISFA na INBATT kama kikosi kinachohusika kutimiza wajibu wake kikamilifu,” alisema Ajak.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x