Fisi auwa mtu mmoja Mtwara

MKAZI wa kijiji cha Chiwambo, kata ya Lulindi, wilayani Masasi, mkoani Mtwara, Haika Mangeja (62), ameuawa  baada ya kuvamiwa na fisi wakati akijaribu kumwokoa mke wake.

Wananchi wa kijiji hicho walifika eneo la tukio na kumkuta fisi huyo akiwa anakula mwili wa marehemu eneo la kichwani na kumuua kwa kutumia silaha za jadi.

Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji hicho, Maimuna Mbaya amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa saba usiku wakati Mangeja na mke wake, Asina Nguriko (49), wakiwa ndani ya nyumba yao wakiota moto na fisi huyo kuwashambulia.

Amesema Mangeja alifariki dunia wakati akimwokoa mke wake ambaye alikuwa akipambana na fisi huyo aliyefika katika nyumba yao.

Habari Zifananazo

Back to top button