Aweso aagiza vifaa vya Maji Mtwara kuletwa mara moja

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso.

WAZIRI  wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso ameagiza vifa muhimu vya kupima ubora wa Maji kwenye maabara ya Maji Kanda ya Mtwara kuletwa mara moja.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Aweso alisema uwekezaji uliofanywa na serikali kwenye ujenzi wa miundombinu uendane na ukubwa wa kazi zinazofanyika katika upimaji wa ubora wa maji.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akitoa maelekezo ya vifaa muhimu vya maji kupelekwa haraka Mtwara

Aweso ametoa maagizo hayo alipotembelea jengo la Maabara ya Maji kanda ya Mtwara na kugundua kuna baadhi ya vifaa vya vipimo muhimu ambavyo hulazimika kufanyika Dar Es Salaam badala ya kumaliza kazi zote za upimaji hapohapo kanda ya Mtwara.

Advertisement