Aweso: Acheni kufanya kazi kwa mazoea

WAZIRI  wa maji, Jumaa Aweso amewataka watendaji kutozoea shida za wananchi na kuhimiza uwajibikaji utakaoleta tija kwa taifa

Amesema ameyasema hayo katika kikao cha dharura cha Menejimenti ya Wizara hiyo  na kuwataka  kujipanga upya na kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kushughulikia changamoto za wananchi katika dhana ya kupata huduma ya Maji.

Amesema, wizara ya Maji inajukumu la  kutekeleza ilani ya chama tawala ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 95 mjini na asilimia 85 vijijini ifikapo 2025.

“Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan inadhamira ya dhati ya kuwaondolea wananchi changamoto ya maji, hivyo kila mtendaji katika sekta ya maji awajibike vyema katika kusimamia jambo hili lenye maslai mapana ya nchi yetu.”Amesema Aweso na kuongeza

“Tuache mazoea kwa shida za wananchi tumepata dhamana ya kuwahudumi, tuwahudumie kwa weledi.” Amesisitiza

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya M aji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba amewakumbusha watumishi kufuata kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa katika kutoa huduma na kuongeza mahusiano baina ya watendaji na wananchi ili kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali.

Habari Zifananazo

Back to top button