WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amempokea Makamu wa Rais wa Benin, Mariam Chabi Talata ambaye amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo alfajiri Julai 25, 2023.
Mariam Chabi ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wanaoendelea kuwasili hapa nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Kuhusu Rasilimali Watu utakaofanyika Julai 25-26, 2023, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.