Aweso atoa maagizo kwa Mamlaka zilizo chini ya Wizara yake

WAZIRI wa maji Jumaa Aweso amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Jamal Katundu kuzisimamia Bodi za Mamlaka za maji 25 ili kuhakikisha zinatekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwemo kutatua changamoto za watumishi sambamba na kusikiliza kero za wananchi badala ya kutegemea viongozi wa juu kutatua changamoto hizo.

Aweso ametoa agizo hilo leo Septemba 25, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya bodi na menejimenti za Mamlaka za maji Tanzania Bara.

Amesema, kwa sasa zoezi la utekelezaji wa miradi mbalimbali linaendelea vizuri changamoto iliyopo ni utoaji wa huduma za uhakika ikiwemo utoaji wa taarifa ya kusitishwa kwa huduma pale inapotokea kuna maboresho.
“Wananchi wanataka huduma wapate kwa wakati haiwezekani mtu anaomba huduma ya kuunganishwa maji sheria inasema ndai ya siku 14 lakini leo mtu ameomba maji miezi sita hajapata huduma, na danadana nyingi mara hakuna vifaa, mwananchi inamuhusu nini ?” Ameswema kwa kuhoji

Aweso pia amekemea tabia ya watumishi wa mamlaka za maji kuwabambikiza bili wananchi na kudai kuwa michezo hiyo imepitwa na wakati.

“Unaposoma mita hakikisha unamshikirikisha mteja, teknolojia imerahisisha, kabla hujamtumia bili ya mwisho muelezee kwa meseji umetumia uniti kadhaa bili hi, hakiki bili yako, kama mtu anasoma saa yake ya mkononi atashindwaje kuosma mita yake?” Amehoji Aweso

Aidha, amehoji wasoma mita wanafuatiliwa vipi iwapo wamefika kwenye eneo na kusoma mita kwa usahihi, iwapo hakuna ufuatiliaji na ndio maana malalamiko ya kubambikwa bili yamekuwa mengi kutokana na wasoma mita kutoa bili kwa kukadiria tu.

Aweso pia amekemea upotevu wa maji ambao na kudai kuwa kuna watumishi wa mamlaka za maji ambao sio waadilifu wanaunganisha maji kwenye baadhi ya taasisi, kampuni na hoteli kinyemela na baada ya kuunganishwa hawalipi bili.

“Mkurugenzi bila aibu anasimama anasema asilimia 40 ya maji yanapotea mtaani, hayo maji mtaani mbona hayaonekani, kama yangekua mtaani nchi nzima ingejaa maji Wizara ya Mifugo isingekuwa inahangaika kuchimba mabwawa, hiyo asilimia 40 itafutwe inapopotelea na hatua stahiki zichukuliwe.”Amesema
Aweso pia ameshangazwa na mamlaka ambazo zimejengewa miradi ya kimkakati ya sh bilioni 50 lakini zimekuwa zikiomba kulipiwa bili ya umeme…; “Mkibebwa shikamana.”

Wakati huo huo, Aweso amezindua bodi za mamlaka 25 zilizoteuliwa hivi karibuni.

“Kwa mujibu wa sheria ya maji na usafi wa mazingira namba 5ya mwaka 2019 sehemu ya 10 na 11 na kanuni ya sita, natamka rasmi bodi za mamlaka 25 zilizoteuliwa zote zimezinduliwa rasmi.

Pia, amesema kwa mujibu wa sheria ya maji namba tano ya 2019 sehemu ya tisa na kanuni ya nne (1) amezipandisha hadhi rasmi mamlaka zilizokua chini ya mamlaka nyingine za Wizara zitajitegemea kama mamlaka kamili kama uandwaji wa bodi zitafuatwa.

“Lakini la msingi wenyeviti wa bodi, wajumbe chini ya sheria za huduma za maji chini ya sheria namba tano ya 2019 bodi ukabidhiwa mamlaka zote za uendeshaji, kushughulikia malalamiko ya watumishi, yaendane sambamba na wateja wetu.

“Watumishi wanachangamoto nyingi sana, ukiachana na maslahi, wakati mwingine kuna mambo ni madogo sana, mtu anataka kusikilizwa, au unakuta baadhi ya mamlaka watumishi wamewekwa kwenye makundi, haiwezakani, wanagawanywa tu kwa makusudi mtumishi hana mkurugenzi mwingine,….; “Unashuhudia kuna kazi anapewa mtu fulani tu, au watu fulani tu lakini watumishi wengine wanakuwa sio sehemu ya mamlaka, tutajenga chuki ambazo hazina ulazima. Niwaombe mkasikilize changamoto za watumishi, changamoto za wateja.

“Ujenzi wa miradi kwa sasa hatuna changamoto, changamoto ninayoiona kwa sasa ni eneo la service delivery, lazima mwananchi katika mamlaka yetu tunayompatia huduma ya maji, huduma yetu iwe ya uhakika, kwamba jukumu la mamlaka ni kumpatia maji ya uhakika, sio mwananchi mwisho wa mwezi unampelekea bili ya maji mwezi mzima hajapata maji si sawa.

“Wakati mwingine unaweza kuona mwananchi hapati maji kwa kuwa kuna maboresho ya mtambo lakini hapewi taarifa, kwa nini msitoe taarifa, tunatengeneza malalamiko ambayo hayana ulazima.”Amesema


“Twendeni tukashughulikie kero za wananchi, inakuwaje meseji zimfikie Rais, kwamba mtu hana maji toka asubuhi wakati sisi tupo, katibu mkuu ikikupendeza weka mifumo mkurugenzi umetumiwa meseji unatakiwa ushughulikie umepata meseji shguhulikia, saa mbili hujashughulikia itaruka mwisho itamfikia katibu Mkuu, Naibu Waziri hadi itanifikia.”Amesisitiza.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x