WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso, amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuunda timu ya wataalamu, ambayo itafanya tathimini ya changamoto ya uhaba wa maji inayoikabili Halmashauri ya Korogwe Mji.
Agizo hilo amelitoa wakati wa ziara yake ya siku katika halmashauri, ambayo imelenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya uhaba wa maji ulipo kwa sasa katika halmashauri hiyo.
Amesema kuwa timu hiyo ya wataalamu iweze kufanya kazi ndani ya siku saba na kuja na majibu ya hatua za kuchukuliwa, ili kusaidia wananchi kuondokana na changamoto ya uhaba wa maji.
Kwa upande wake Mkurungenzi wa Mamlaka ya Maji mji Korogwe, Sifael Masawa amesema kuwa wilaya hiyo inahitaji Sh Mil 825.3 kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maji, ikiwemo uchimbaji wa visima saba.