Aweso: Mita za maji ziwe kama luku za umeme

PWANI: MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imesaini mikataba mitatu yenye thamani ya Sh Bilioni 48 ya utekelezaji wa miradi ya Maji Pangani, Kwala na Kigamboni.

Miradi hiyo yenye thamani ya Sh bilioni 48 itanufaisha wananchi 183,519 ikitekelezwa kwa kutumia fedha kutoka serikali Kuu.

Wakandarasi wa miradi hiyo ni China Civil Communication and Engineering Company ( CCCEC), Shanxi Construction Engineering Corporation and Mineral Company (SCECMC) chini ya usimamizi wa Wahandisi wa ndani wa Mamlaka.

Akichanganua miradi hiyo leo Desemba 15, 2013 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Kiula Kingu amesema mradi wa Kwalq
unatarajiwa kuwanufaisha wananchi 7,901 wa maeneo ya Mji wa Kwala na vitongoji vyake, Bandari Kavu, viwanda vikubwa na vidogo vipatavyo 200 na vile vya Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwanj, SGR Marshalling Yard.

Amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa matenki ya juu ya kuhufadhi maji Lita milioni 1.5, ujenzi wa kituo cha kusukuma maji chenye tenki la kupokelea maji lenye mita za ujazo 1,000 na kazi ya ufungaji pampu tatu za kusukuma maji pamoja na ufungaji mita.

Pia utahusisha ulazaji wa bomba Kuu la kusafirisha maji la nchi 16 na 12 kwa umbali wa kilomita 25.1na ulazaji wa bomba la usambazaji maji la nchi nane na nne kwa umbali wa kilomita 46.4

Mradi huu wa Kwala utagharimu Sh bilioni 23.6 bila VAT ukitekelezwa kwa kutumia fedha kutoka Serikali Kuu.

Aidha, mradi wa Pangani utahusisha ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji la ujazo wa Lita milioni 6, tanki la kusukuma maji lenye mita za ujazo 540 ufungaji wa pampu na Mita.

Pia, utahusisha ulazaji wa mabomba na utakua na uwezo wa kusafirisha maji kiasi cha lita za ujazo milioni 12 kwa siku ambayo ni mahitaji ya miaka 20 ijayo na kunufaisha wananchi 14, 868 ukigharumu sh bilioni 8.9

Mradi wa Maji Kimbiji mpaka Chuo cha uhasibu (TIA) utakua na uwezo wa kusafirisha maji kiasi cha Lita za ujazo milioni 21 na kunufaisha wananchi 160,750 wa maeneo ya katikati ya jiji, eneo la Tazara, Ukonga hadi Gongo la Mboto. Mradi huo utagharimu sh bilioni 12.6 na unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali kuu.

Kwa upande wa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Dawasa kuwasimamia wakandarasi hao kwa karibu ili mradi huo ukamilike kwa wakati kabla ya 2025.

Pia, ametaka utakapokamilika wananchi wafungiwe kwa wakati.

“Kusiwe na longolongo sijui hakuna mita, fitting zimeisha sitaki kusikia, tutakuja kugombana wananchi wameteseka muda mrefu isitokee mtu anataka kuunganishwa mnataka kidogo dogo, mi ni kijana ukizingua nakuzingua.” amesema

Aidha, amesema ni haki ya Mwananchi kupata maji na kulipia maji ni marufuku kumbambikizia Mwananchi maji, haiwezekani Mwananchi ambae ametumia maji ya sh 10,000 akapewa bili ya sh 150,000 kama ana kiwanda.

“Wasoma mita wawe waaminifu na wenye maadili, wanaposoma mita zao lazima wamshirikishe Mwananchi, msoma mita asipokushirikisha Mwananchi toa taarifa. Tutawachukulia hatua wote watakaobainika kuchafua jina la Mamlaka, ” amesema.

Aidha, amesisitiza kuwa Mita za maji ziwe kama luku za umeme.

“Muda muafaka wa Wizara na Mamlaka zake kuhakikisha zinafunga luku za maji,
Mwananchi atatumia kulingana na hela yake, hakutakuwa na nongwa, ” amesema

Habari Zifananazo

Back to top button