Aweso: Yanga haishikiki, Simba tuvumilie

DODOMA:Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameipongeza Timu ya Yanga kwa kuendelea kuwa katika kiwango bora kwenye michuano mbalimbali inayoshiriki.

Akizungumza leo bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025, Aweso amesema kama mpinzani wa kweli ni lazima akubali kile kinachofanywa na timu hiyo kwa sasa.

“Mh Spika kwakuwa tupo katika ulimwengu shindani ni vyema ukampongeza mpinzani, niipongeze Yanga kwa kuendelea kusambaza maji nchi nzima…, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kwa kweli kwa Yanga hii haikamatiki wala haishikiki” amesema Aweso.

Pia Kiongozi huyo ameitaka Klabu ya Simba kuendelea kuwa na uvumilivu kwani ni suala la muda tuu watarejea kwenye ubora wao.

“Niseme wazi kabisa kwa upande wetu wa Msimbazi tuendelee kujipanga na kuangalia jinsi ya kurejea katika ubora, tutajipanga ukubwa ni kuvumilia, tuendelee kuvumilia naimani haya ni mapito tutaendelea kufanya vizuri” amesema Aweso.

Habari Zifananazo

Back to top button