Azam bado waiwazia Yanga

KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala amesema walitamani kukutana na Yanga kwenye hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC),  ili kulipa kisasi cha kufungwa kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na HabariLEO, Kocha huyo ameeleza kuwa wanapocheza na Yanga kuna sehemu ndogo huwa wanakosea na kushindwa kupata ushindi,  hivyo aliamini kama wangekutana kwenye michuano hiyo ilikuwa ni sehemu sahihi ya kulipa kisasi chao.

“Tunaweza kukutana na Simba kama atashinda mchezo wake dhidi ya Ihefu, siyo mbaya lakini nilitamani kama tungekutana na Yanga, kwa sababu ndio wamechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza malengo yetu ya ubingwa msimu huu,” amesema Kally.

Azam FC juzi ilitinga hatua ya Nusu Fainali ya michuano hiyo, baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button