Azam FC ya Tanzania imepangwa kucheza na Bahir Dar FC ya Ethiopia katika hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mshindi kati yao atakutana na Club Africans ya nchini Tunisia.
Singida Fountain Gate ya Tanzania imepangwa kucheza na JKU ya Zanzibar katika hatua ya kwanza ya mtoano Kombe la Shirikisho Afrika.
Mshindi kati yao atakutana na Future FC ya nchini Misri.