Azam FC haitanii suala la ubingwa

Kuelekea kuanza kwa mechi za mzunguko wa pili Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC, Kally Ongala leo Desemba 13 amesema wamejipanga kucheza kwa umakini mkubwa ili kutimiza lengo lao la ubingwa msimu huu.

Azam FC itaanza mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu wakiwa ugenini uwanja wa Kaitaba kwa kucheza na Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Desemba 16.

Akizungumza na SpotiLeo, kocha huyo ameeleza kuwa ushindi walioupata katika mechi nane mfululizo zilizopita umechangia kuimarisha viwango vya wachezaji wake na kucheza kwa kujiamini zaidi bila kujali kuwa wapo ugenini.

“Najua hautokuwa mchezo rahisi kwakua tutakuwa ugenini, Kagera Sugar ni timu nzuri inafundishwa na kocha mwenye mbinu bora lakini Azam kwa sasa tumeimarika zaidi tofauti na tulivyoanza mzunguko wa kwanza lengo letu ni kuendeleza rekodi yetu ya kushinda mpaka mwisho wa ligi ikiwezekana,” amesema Kally.

Kocha huyo amesema wachezaji wake wanatambua hilo na anachofurahi ni kuona kila mmoja wao amekuwa akicheza kwa kujituma kuhakikisha timu hiyo inatimiza malengo ambayo wamedhamiria kuyafikia mwishoni mwa msimu huu.

Azam FC imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikikusanya pointi 35 huku ikifuatiwa na Simba iliyopo nafasi ya tatu na pointi zao 34 Yanga wakiwa nafasi ya kwanza kwa kuwa na pointi 38.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
gate io 交易所
9 days ago

好文章!你的文章对我帮助非常大。谢谢!你赞同我这么做吗?我想把你的文章分享到我的网站:
gate io 交易所

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x