Azam FC yapigwa faini Sh milioni 1

KLABU ya Azam imetozwa faini ya Sh milioni 1 na Bodi ya Ligi (TPLB) kwa kosa la shabiki wake mmoja kuonekana akimwaga kitu mfano wa unga uwanjanin wakati wa mapumziko katika mchezo dhidi ya Singida FG.

Taarifa iliyotolewa leo Machi 9, 2024 na TPLB, imefafanua kuwa adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 41:5 ya ligi kuu kuhusu udhibiti kwa wachezaji.

TPLB pia imeeleza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amepewa onyo kwa kosa la kuingia kwenye chumba cha kuvalia katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC na kuzungumza na wachezaji dakika chache kabla ya mchezo huo.

Mamlaka hiyo imeleeza adhabu hiyo imetokana na kanuni ya 17:50 na 17:60 za ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Habari Zifananazo

Back to top button