Azam yaanza kugawa ‘Thank You’

BEKI Daniel Amoah amekuwa mchezaji wa kwanza kuachwa na klabu ya Azam.

Klabu za madaraja mbalimbali nchini zipo katika harakati za kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano baada ya dirisha la uhamisho na usajili kufunguliwa mwezi huu.

“#ThankYou Ahsante kwa utumishi wako wa miaka nane ya nguvu ukiipigania nembo ya klabu yetu, aliyekuwa nahodha wetu, Daniel Amoah. Thank you for your memories, Amoah! 👍🤝👏,”imesema taarifa ya Azam kupitia mitandao yake ya kijamii.

Azam imeshika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyofikia tamati Mei 28, 2024 hivyo kukata tiketi kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Habari Zifananazo

Back to top button