MPAKA sasa wachezaji wawili wa Yanga wameonja ladha ya michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa kuanza katika timu zao.
Mchezo wa mapema uliopigwa leo saa 11, kati ya Bukinafaso Mauritania, kiungo wa Yanga SC, Stephen Aziz Ki alianza kwenye kikosi cha Bukinafaso.
Mchezo usiku, kati ya Mali na Afrika Kusini, kipa Djigui Diarra pia ameanza kwenye kikosi cha mali.
Bukinafaso na Mali wote wameshinda michezo yao.