Baada ya kukutana na Harmonize Rayvany abadili gia angani
DAR ES SALAAM; Siku kadhaa nyuma msanii wa muziki wa Bongo fleva, Raymond Shaban ‘Rayvany’ alitangaza kuachia EP yake tarehe sawa na ile aliopanga msanii mwenzake ,Rajab Abdul Kanali maarufu Harmonize kuachia Album yake ya VisitBongo Novemba 24,2023.
Rayvany baada ya kukutana na Harmonize kwa ajili ya kufuata tuzo yake aliyochukuliwa na msanii huyo huko nchini Marekani, amefunguka kuhairisha kutoa EP yake Novemba 24 na kusema kuwa ataiachia Disemba 1,2023.