Baadhi ya Kampuni Ulaya zaomba msamaha vikwazo Urusi

© Getty Images

KAMPUNI kadhaa za Kiestonia zimeomba msamaha wa muda wa vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi ili kuendelea kuagiza bidhaa za mafuta kutoka Urusi

Shirika la utangazaji la serikali limeripoti likinukuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Estonia kuwa kampuni 28 zingependa kuendelea kuagiza bidhaa za mafuta kutoka Urusi, licha ya vikwazo vilivyowalazimu kusitisha mikataba iliyopo na makampuni ya mafuta ya Urusi ifikapo Oktoba 10. 

Orodha hiyo inajumuisha kampuni ya mafuta Trafigura na Shirika la reli ya serikali ya Estonia, Operail.

Advertisement

“Nina hakika kwamba umma wa Estonia una nia ya kujua ni kampuni gani za Estonia zimeomba msamaha wa mpito ili kuendelea na biashara ya mafuta na Urusi,” ERR ilimnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Estonia Urmas Reinsalu akisema.

EU iliweka vikwazo vya sehemu kwa mafuta ya Urusi katika kifurushi chake cha sita cha vikwazo vilivyotangazwa mapema mwezi Juni.

 

/* */