Baba atupa maiti ya kichanga jalalani

BABA mmoja asiyefahamika ameripotiwa kutupa mwili wa mtoto mchanga jalalani kando ya Uwanja wa CCM Kalangalala mjini Geita, muda mfupi baada ya kukabidhiwa mwili kwa ajili ya mazishi.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Inspekta Edward Lukuba amethibitisha kupokea taarifa hiyo Januari 4, 2023, majira ya saa tano asubuhi na kueleza mtuhumiwa bado hajajulikana.

Amesema askari walifika eneo la tukio na kuchukua mwili wa mtoto na kuurejesha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, ambapo mwili huo ulitambuliwa na madaktari na kuthibitisha mtoto alikuwa amefariki.

Amemtaja mama wa mtoto ni Emanuelina Merikioli, ambaye alikuwa amekabidhiwa mwili huo kwa ajili ya taratibu za mazishi ambaye naye alikabidhi mwili kwa mtu anayetajwa kuwa baba wa mtoto.

Shuhuda wa tukio, Baraka Mathayo amesema alimuona mwanaume huyo akitupa boksi lenye kanga na kisha kukimbia na alipofika kutazama kilichotupwa alishangazwa kuona kilichomo ni mtoto.

 

Habari Zifananazo

Back to top button