Baba mbaroni akidaiwa kutaka kumnajisi bintiye

POLISI Mkoa wa Mwanza inamshikilia Godbless Mushi (39), ambaye ni muuza spea za magari, mkazi wa Shibula wilayani Ilemela kwa tuhuma za kujaribu kumbaka bintiye mwenye umri wa miaka (5), mwanafunzi wa chekechea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroard Mutafungwa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 2, mwaka huu katika Mtaa na Kata ya Shibula.

Amesema wakati mtoto huyo akiwa amelala chumbani kwenye kitanda cha wazazi wake, huku mama yake akiwa anaendelea na shughuli zake za kawaida nyumbani, ndipo mtuhumiwa alipojaribu kumfanyia vitendo vya udhalilishaji wa kingono mtoto huyo.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Habari Zifananazo

Back to top button