Baba mbaroni vifo vya wanawe

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linamshikilia Makeremo Nyasa Luhaga, mkazi wa kitongoji cha Kitete kutokana na tukio la vifo vya watoto wake wawili, baada ya kunywa vitu vinavyodhaniwa ni dawa za kienyeji.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamini Kuzaga, imeeleza kuwa Februari 19, 2023 majira ya saa 2 asubuhi, jeshi  hio lilipokea taarifa ya vifo vya watu wawili, baada ya kunywa dawa ya kienyeji waliyopewa na mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina moja la Galwinzi.

Waliofariki baada ya kunywa dawa hiyo ni Raphael Makeremo (26) na Mafunda Makeremo (18), wakazi wa Kitete, wakati watu wengine watatu Nchambi Lusangija (50), Manyilizu Kulyehelwa (07) na Njile Makeremo (18) wakazi wa Kitete wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa matibabu baada ya kunywa dawa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hili ni imani za kishirikina kutokana na watoto wa familia ya Makeremo Nyasa Luhaga kusumbuliwa na maradhi ya tumbo na vichomi kwa muda mrefu, hivyo kuamini matatizo hayo yanatokana na kurogwa.

Habari Zifananazo

Back to top button