Baba wa Yannick Bangala afariki dunia

BABA mzazi wa kiungo wa Azam FC, Yannick Bangala aitwaye Bangala Denis amefariki dunia, taarifa ya Azam FC imethibitisha.

Klabu hiyo imechapisha taarifa hiyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Taarifa ya Azam iliandikwa: “Uongozi wa Azam FC umepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha baba yake mzazi nyota wetu, Yannick Bangala, Bangala Denis, kilichotokea jana.”

Advertisement

“Azam FC tunatoa salamu za rambirambi kwa familia ya Bangala, ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huu.”