Babu adaiwa kumnajisi mjukuu wa miaka 5

Babu adaiwa kumnajisi mjukuu wa miaka 5

JESHI la Polisi, mkoani Simiyu linamshikilia, Mahona Mboje (65), Mkazi wa Kijiji cha Mpindo, Kata ya Sanga, wilayani Maswa kwa tuhuma za kumnajisi mjukuu wake mwenye umri wa miaka mitano aliyekuwa akiishi naye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda, anasema mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 9, 2022 saa 10 jioni, nyumbani kwake.

Kamanda amesema, wakati mtuhumiwa akitekeleza kitendo hicho, mkewe ambaye ni bibi wa binti huyo alikuwa ameenda kuchunga mifugo.

Advertisement