WASANII kutoka nchini DR Congo, Babu Seya na bendi ya FM Academia wanaongozwa na Nyoshi All Sadati kuupamba usiku wa Rhumba Di Rumba Machi 30 mwaka huu katika ukumbi wa Wehe House uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Habari Leo jijini Dar es Salaam, Muandaaji wa tamasha hilo, ambaye pia ni Rais wa Jumuiya ya Wacongo nchini Jean Paul amesema tuliona Uhuru wa Congo usipite patupu utakuwa wa kitofauti na burudani za kutosha.
“Haikuwa rahisi kwasababu sio Wacongo wote wako kwenye bendi moja wamesha sambaratika bendi tofauti tofauti lakini tumefanikiwa kuwakutanisha katika usiku wa Rhumba Di Rumba wataimba kwa pamoja.” amesema Paul
kwa niaba ya bendi hiyo FM Academia Nyoshi El Sadati amesema kuwa usiku huo kubwa zaidi ni kusherekea siku ya uhuru wa Wacongo huko nchi ya DRC Congo.
“Sisi ndo bendi na wakali wa muziki huu wa dance rasmi tunatarajia kutoa burudani kabambe na ya ainayake pale Werehouse Masaki jijini Dar es Salaam.
“Pamoja tunasherekea Uhuru wa Wacongo ila tupo nchini Tanzania hivyo hatutakuwa peke yetu tunatarajiwa kusindikizwa ambao watatumbuiza nasi ni pamoja na Twanga Pepeta, Akudo impact na nyingine nyingi.” amesema Nyoshi